NGUVU YA ELIMU KATIKA KIPAJI.
Na Mwl. Dominick Diwani
Katika miaka ya kabla ya maendeleo ya viwanda (Kabla ya miaka ya 1750), Ardhi ilikuwa ni kipimo cha utajiri, ambapo wamiliki wa ardhi walikuwa ndio wakuu wa nchi, lakini baada ya maendeleo ya viwanda Ulaya Umiliki wa viwanda ndio ilikuwa kigezo cha utajiri.
Ulimwengu umebadilika, dunia imewekeza katika maarifa, elimu imekuwa moja kati ya vigezo vikuu vya kipimo cha utajiri. Uwepo wa taarifa katika akili ya mwanadamu umuwezesha kuaamua namna ya kuishi, Jamii na serikali za kimataifa inafanya jitihada kila kukicha katika kuwezesha maendeleo ya elimu duniani, ikiwa ni kama nyenzo ya kupambana na umasikini duniani.
Mbali na Elimu, Kipaji Kimekuwa ni sehemu ya nyenzo ya kupambana na umasikini. Inashuhudiwa duniani kote namna wanamichezo, wasanii na watu mbali mbali wakitumia vipaji vyao katika kupambana na umasikini kwa kujitafutia kipato.
Chachu hii imeungwa mkono na wanaharakati wengi wa masuala ya kijamii na uchumi. Mbali na hilo, imeathiri kwa namna moja ama nyingine ya hitaji la elimu katika jamii yetu, (Tanzania). Watu mbali mbali, wanaotambulika kama "Wahamasishaji" wamekuwa wakisisitiza utambuzi wa vipaji kama njia ya kupambana na umasikini wakisahau au kutolipa kipaumbele suala la utambuzi wa elimu.
Malezi ya wazazi wengi wa kiafrika bado yanaakisi kuelimika na kuwa na maisha mazuri. Wazazi wengi husisitiza watoto wao kusoma ili kujipatia kazi zenye heshima nchini kama udaktari, uanasheria, uongozi na usimamizi na kazi nyinginezo, huku wakilitupilia mbali suala la kuelimika na kuuaga ujinga.
Wakiongozwa na falsafa hiyo, wanafunzi wengi wamekuwa wakihusianisha watu walioelimika na utajiri au kipato wapatacho, lakini vile vile suala la kumaliza masomo na kupata ajira, huku wakilitambua kama janga la dunia nzima, na kuona namna watu wengi walio na elimu wakitapa mtaani kujitafutia riziki zao za kila siku kwa shida tofauti na matarajio yao.
Hii huathiri saikolojia ya wanafunzi katika kulitambua dhumuni la elimu, na hivyo kuwafanya waanze kutambua vipaji vyao mapema.
Suala hili ni zuri, lakini wajibu wa wazazi, walimu na jamii kwa ujumla ni kuwakumbusha vijana wetu, nguvu ya elimu katika kipaji, upatikanaji wa elimu husaidia.

- Kufanya kipaji kitumike kulingana na wakati na mahala
- Kuendeleza nguvu ya kujitegemea kwa mtu binafsi.
- Humuwezesha mtu kutambua thamani ya kipaji chake na kustahimili/kukabili mazingira yote yanayoweza kutishia kipaji chake
- Kumuwezesha mtu kujitofautisha na wengine wenye kipaji kama chake.
- Kutambua fursa kwa kiwango cha dunia nzima.
Vipaji vingi vinakufa kwa sababu wenye navyo hawana uhuru wa kimawazo, wanashindwa kujitofautisha na wengine na vile vile hunyonywa kwa sababu ya kulaghaiwa na watu wenye fikra pana na wenye ushawishi.
USHAURI: Tutambue vipaji vya watoto wetu vile vile tusisitize elimu katika kipaji husika, ili kuboresha maana kamili ya elimu.

Comments
Post a Comment