Posts

NGUVU YA ELIMU KATIKA KIPAJI.

Image
Na Mwl. Dominick Diwani Katika miaka ya kabla ya maendeleo ya viwanda (Kabla ya miaka ya 1750), Ardhi ilikuwa ni kipimo cha utajiri, ambapo wamiliki wa ardhi walikuwa ndio wakuu wa nchi, lakini baada ya maendeleo ya viwanda Ulaya Umiliki wa viwanda ndio ilikuwa kigezo cha utajiri. Ulimwengu umebadilika, dunia imewekeza katika maarifa, elimu imekuwa moja kati ya vigezo vikuu vya kipimo cha utajiri. Uwepo wa taarifa katika akili ya mwanadamu umuwezesha kuaamua namna ya kuishi, Jamii na serikali za kimataifa inafanya jitihada kila kukicha katika kuwezesha  maendeleo ya elimu duniani, ikiwa ni kama nyenzo ya kupambana na umasikini duniani. Mbali na Elimu, Kipaji Kimekuwa ni sehemu ya nyenzo ya kupambana na umasikini. Inashuhudiwa duniani kote namna wanamichezo, wasanii na watu mbali mbali wakitumia vipaji vyao katika kupambana na umasikini kwa kujitafutia kipato. Chachu hii imeungwa mkono na wanaharakati wengi wa masuala ya kijamii na uchumi. Mbali na hilo, imeathiri kwa namna ...